Mwenyekiti wa Kazi Mashinani Amuomboleza Raila Odinga, Asema Alikuwa Malaika wa Wokovu kwa Kenya.

Nairobi, Oktoba 16, 2025 — Mwenyekiti wa kitaifa wa Kazi Mashinani, ambaye pia anaongoza Team Rao County Coordinators, Bw. Joachim Maragia, ameungana na Wakenya na dunia nzima kuomboleza kifo cha Rt. Hon. Hayati Raila Amollo Odinga.

Bw. Maragia amemuelezea marehemu Raila Odinga kama malaika aliyetumwa kuikomboa Kenya, akisema kifo chake kimewashtua wengi ndani na nje ya taifa. Alisema Raila alikuwa mtu mwenye moyo wa upendo, mpole, na aliyesikiliza kila mtu bila kujali hadhi au nafasi yao katika jamii.

“Raila alikuwa kiongozi wa kipekee, mwenye hekima na busara. Aliamini katika haki, usawa, na umoja wa Wakenya wote. Tumepoteza taa ya matumaini,” alisema Maragia kwa huzuni.

Aidha, Bw. Maragia ametoa wito kwa wanachama wa Team Rao County Coordinators kukutana kuanzia siku ya Ijumaa katika Jumba la Jaramogi Oginga Foundation ili kujadili zaidi namna ya kumuenzi kiongozi huyo mashuhuri.

Maragia amehitimisha kwa kusema kuwa urithi wa Raila Odinga utaendelea kuishi milele katika mioyo ya Wakenya wote walioamini katika maono yake ya Kenya huru, yenye haki na usawa.

Previous Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *